19 February 2018

February 19, 2018

WAZIRI MKUU AMPA SIKU TATU DED AJIELEZE AMEPELEKA WAPI MILIONI 350

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati aeleze amepeleka wapi zaidi ya sh milioni 350 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali.


Ametoa agizo hilo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.


Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumia kuona fedha inazopeleka katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharamia miradi na kulipa madai ya watumishi zinatumika kinyume na maelekezo.

Alisema miongoni mwa fedha hizo ni sh. milioni 451.47 za miradi ya miradi ya maendeleo (CDG), ambapo zilizotumika ni sh. milioni 221.9 tu.” Namtaka Mkurugenzi na Muweka hazina wa Halmashauri hii Bw. Peter Molel tarehe 21 waje Mwanza wanieleze walikopeleka fedha hizo.”

Waziri Mkuu amesema fedha zingine ni sh. milioni 50 za ziizotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi kama likizo ambapo zililipwa sh. milioni 13 na zingine hazijulikani zilipo.

Pia Serikali ilitoa sh. milioni 65 za kugharamia mradi wa umwagiliaji wa Bugorola ambazo nazo hazijulikani zilipo pamoja na sh. milioni 84 zilizotolewa kwa ajili ya kulipa motisha kwa walimu ambapo zilizolipwa ni sh. milioni 60 tu.

“Kama mlidhani Ukerewe ni sehemu ya kutafunia fedha za umma mmekosea kwa sababu Serikali haiwezi kuvumia haya, Mkurugenzi umeaminika na kupewa dhamana ya kusimamia rasilimali za umma lakini unafanya tofauti.”


Waziri Mkuu amesisitiza kwamba lazima viongozi hao wahakikishe fedha zinazopelekwa na Serikali katika Halmashauri zao zikiwemo za utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, uvuvi zinatumika kama ilivyoelekezwa na si vinginevyo.


Pia Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza asimamie utendaji wa viongozi na watumishi katika wilaya zote za mkoa huo na kisha kutoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Bw. John Mongella.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo wasikubali kugawanywa kwa sababu ya maslahi ya watu ambayo hayana tija kwao na hata kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kubaini kuwepo kwa mgogoro kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Bahari pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. George Nyamaha ambao wamekuwa wakiwagawa watumishi.

Amewataka viongozi hao kurekebisha tofauti zao kwa sababu mgogoro wao umesababisha watumishi kugawanyika, hivyo kuwaumiza wananchi wa wilaya ya Ukerewe kwa kushindwa kuwahudumia vizuri jambo ambalo halikubaliki.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 18, 2018.
February 19, 2018

MWANAMKE ACHOMWA MOTO NA WAGANGA WA JADI ILI APATE UJAUZITO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, linawashikilia waganga wa jadi wawili ambapo mmoja ni mkazi wa Kijiji cha Obwere na Michael Jacob wa Omuga kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumuunguza moto, Emiliana Thomas anayeishi Kijiji cha Omuga wilayani Rorya.


Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Henry Mwaibambe alisema jana kuwa, majeruhi huyo ambaye ni mwanamke anayesumbuliwa na tatizo la kutopata ujauzito, waganga hao walimwaminisha kuwa ataupata.


Alisema walimwambia ili apate mtoto ni mpaka kuku imwagiwe mafuta ya taa na iteketezwe moto huku mama huyo akiwa ameishikilia mikononi.


Kamanda alisema baada ya waganga hao kuwasha moto ulimunguza na kumsababishia majeraha.


Mwaibambe alisema, awali waganga hao walimweleza mwanamke huyo kuwa anasumbuliwa na mashetani ndani ya tumbo na ndio yanayomfanya asizae.


Alisema walimweleza kwamba kuku ikiteketea ikiwa mikononi mwake atakuwa ameondokana na mashetani, hivyo ni lazima iteketezwe.


Kamanda huyo alisema baada ya waganga hao ‘kumsomesha’ mwanamke huyo alikubali na ndipo walipoimwagia mafuta ya taa kuku hiyo na kuwasha moto kwa kibiriti uliolipuka na kumjeruhi kifuani na mikononi.


Mwaibambe aliongeza kuwa, hali ya mama huyo ni mbaya na anaendelea na matibabu katika Hospital ya Kowak wilayani humo.

Mmoja wa waganga hao wa jadi, Jacob alisema tukio hilo ni ‘bahati mbaya’.

“Alikuja akiomba tiba, sasa kwa bahati mbaya mafuta yalikuwa yamemumwagikia mikononi na mikono ya nguo aliyokuwa amevaa ilikuwa hadi mikononi, wakati tumewasha moto ndipo ukamuunguza,” alisema Jacob.


Akizungumza na gazeti hili, mwakilishi wa Chama cha Tiba Asili mkoani Mara, Jacob Matiko alilaani kitendo hicho kuwa hakiendani na taratibu za tiba na kinakiuka sheria inayozuia vitendo hivyo huku akiwataka waganga kutofanya utapeli iwapo hawawezi kufanya tiba kama matabibu asili.


Wakati huohuo, polisi inawashikilia watu wawili kutoka Ethiopia kwa kuingia nchini bila vibali.


Mwaibambe alisema katika tukio hilo waliwakamata pia Watanzania wawili ambao walikuwa wakiwasafirisha raia hao wa kigeni akiwamo na Pasaka Meng’anyi mkazi wa Buhemba mjini Sirari wilayani Tarime.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Meng’anyi alieleza kuwa alipewa kazi ya kuwapokea raia hao kutoka Stendi ya Tarime hadi Mwanza na wakifika mjini humo kuna mtu atakayewapokea.


Alisema ili kufanikisha kazi hiyo alilipwa Sh300,000 huku mwenzake akiahidiwa kulipwa 100,000 ambazo bado hajalipwa baada ya kuwatoa Sirari hadi Stendi ya Tarime.

14 February 2018

February 14, 2018

Katibu wa Chadema kuzikwa Ijumaa

Mwili wa aliyekuwa Katibu wa Chadema Kata ya Hananasif jijini Dar es Salaam, Daniel John unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Iringa kwa maziko. John ambaye ni mpigapicha maarufu Hananasif aliuawa na watu wasiojulikana na mwili wake uliokotwa jana kwenye fukwe za Coco. Akizungumzia maandalizi ya mazishi ya kiongozi huyo, mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko ambaye anasimamia kampeni za Chadema katika kata hiyo amesema marehemu atasafirishwa kesho na kuzikwa Ijumaa.

 Matiko amesema vikao vya kukusanya fedha kwa ajili ya kusafirisha mwili wa mwanachama wao huyo vinaendelea kufanyika na kesho wanatumaini kusafirisha kwenda Mafinga mkoani Iringa. "Tumewasiliana na familia ya marehemu wametaka ndugu yao akazikwe Iringa. Tunafanya jitihada za kukusanya fedha ili kufanikisha mazishi ya kiongozi wetu," amesema.

Mbunge huyo amelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya watu waliohusika kukatisha maisha ya kijana huyo Matiko amebainisha kuwa ana uhakika asilimia 100 kwamba hayo ni mauaji ya kisiasa kwa sababu marehemu alitishiwa maisha na watu ambao wanafahamika.

 Akizungumzia mazingira ya kifo cha mumewe, mjane wake, Paulina Vitalis amesema kuna watu walikwenda nyumbani kwake Jumapili, Februari 11 kumuulizia mumewe akawaambia hayupo. Amesema baada ya kuwajibu hivyo waliuliza tena kuwa muda anaorudi nyumbani, akawajibu saa nne usiku Amesema siku hiyo mumewe hakurudi nyumbani mpaka jana Jumanne ambapo alipata taarifa kwamba mumewe alikuwa ameuawa na mwili kuokotwa kandokando ya fukwe za Coco. "Hakuna siku mume wangu aliwahi kuniambia kwamba anatishiwa maisha, lakini Jumatatu watu ndio waliniambia kwamba kuna watu walikuwa wanamtafuta sana," amesema mwanamke huyo ambaye alizaa mtoto mmoja na mwanasiasa huyo.

Akizungumza kwenye msiba huo nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Kawawa , Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuuawa kwa John ni njama za washindani wao kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni ili kuwapunguza nguvu.

Amewataka viongozi na wanachama wa Chadema kutorudi nyuma, bali waendelee na kampeni kama kawaida wakati watu wachache wakiratibu shughuli za mazishi ya kiongozi wao. "Wenzetu wameamua kuua ili tu washinde uchaguzi huu, tusikubali kuvurugwa na msiba tukasahau uchaguzi. Tukifanya hivyo, lengo lao litakuwa limetimia," amesema Mbowe.

Amewataka wanachama wawe watulivu wakati shughuli za kupumzisha mwili wa marehemu zikiendelea na washirikiane na viongozi wanaoratibu mazishi katika kufanikisha suala hilo. Awali, akizungumza kwenye msiba huo, mbunge wa viti maalumu, Susan Lyimo amesema hali ya kisiasa nchini sasa si nzuri kwa sababu viongozi hawataki kukosolewa. "Hawataki kuona kiongozi anatoka Chadema ndio maana wanatumia nguvu nyingi kuwadhibiti.

Mtakumbuka Alphonce Mawazo aliuawa, Tundu Lissu naye alipigwa risasi na kunusurika kuuawa," amesema Lyimo. 
February 14, 2018

Nyoso afungiwa mechi 5 kwa kosa la kumpiga shabiki

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza kumfungia mchezaji Juma Nyoso kutoka klabu ya Kagera Sugar kwa kosa la kupiga shabiki baada ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Ameadhibiwa kwa kuwa vitendo kama hivyo ni kinyume na kanuni za ligi kuu zinazozungumzia mchezo wa kiungwana.
Kamati imemtia hatiani Juma Nyoso kupitia kanuni za ligi kuu na katiba ya TFF lakini ilipokea taarifa za nyuma za Nyoso kwamba aliwahi kuadhibiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Kwa hiyo kamati imemfungia Nyoso mechi tano pamoja na faini ya shilingi 1,000,000 (milioni moja).
February 14, 2018

Baba aliyemkatisha masomo mwanae na kumuozesha jela miaka 30

Baba mlezi wa mwanafunzi mmoja wa darasa la pili wilayani Same mkoani Kilimanjaro amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mtoto huyo kukatisha masomo na kuolewa.
Akizungumzia tukio hilo Afisa ustawi wa jamii wilayani Same, Lucy Venance amesema baadhi ya wazazi wamekuwa mstari wa mbele kukwamisha jitihada za watoto wao kuendelea na masomo.
Katika kipindi cha mwaka 2017, Halmashauri ya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imepokea matukio manne ya watoto wa kike kutaka kuozeshwa ambapo watuhumiwa watatu walitoroshwa licha ya watoto waliofanyiwa ukatili huo kuokolewa.
Kituo cha Ushauri Same ambacho kinamhudumia mwanafunzi huyo kwa sasa kimeitaka jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu na kutimiza ndoto zao.
TBC ilizungumza na Mwendesha mashtaka katika mahakama ya wilaya ya Same, Ancibetus Kechoka ambaye amekiri kupokea shtaka hilo ambapo mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka thelathini huku katibu tawala wa wilaya ya Same, Sospeter Magonera akielezea azma ya kuendelea kuwatafuta wazazi wa mtoto huyo.
February 14, 2018

Majira ya joto huzalisha vijidudu vinavyo sababisha ugonjwa wa kuhara

Majira ya joto ni kipindi ambacho vijidudu mbalimbali vya tumboni vinapozaliwa, kwa hiyo majira hayo pia ni kipindi ambacho watu wengi wanapata ugonjwa wa kuhara. Katika kipindi hiki, tutawaelezeni jinsi ya kupambana na ugonjwa huo.
Bw. Li Jin ni mwalimu wa michezo katika shule ya sekondari, ana afya nzuri lakini katika mwezi mmoja uliopita alikuwa anasumbuliwa sana na ugonjwa wa kuhara.
Zamani Bw. Li Jin aliwahi kupata ugonjwa wa ghafla wa tumbo, na nusura apoteze maisha yake. Kwa hiyo safari hii baada ya kupata ugonjwa wa kuhara, mara moja alitumia mwenyewe dawa za kuangamiza vijidudu kwa siku mbili, lakini hazikusaidia hata kidogo. Bw. Li Jin alilazimishwa kwenda hospitali na kupigwa sindano kwa siku tano mfululizo, hatimaye hali yake iliboreka. Lakini baada ya siku chache tu, usumbufu wake ulirejea tena. katika siku hizo, uzito wake ulipungua kwa kilo 10 hivi.
Mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya tumbo katika hospitali ya Xiehe ya Beijing profesa. Qian Jiaming alisema, watu wengi wana mtizamo kama Bw. Li Jin kwamba dawa za kuangamiza vijidudu zinaweza kutibu vizuri ugonjwa wa kuhara, kwa kweli mtimazo huo ni kosa. Profesa Qian alisema, ugonjwa wa kuhara una vyanzo vingi, kwa jumla vinagawanyika kwa aini mbili, yaani ugonjwa wa kuhara uliosababishwa na vijidudu na wadudu wa tumboni, aina nyingine inatokana na kupatwa na baridi, utapiamlo na magonjwa mbalimali sugu kama vile magonjwa ya ini, kongosho n.k.
Profesa Qian alisema, dawa za kuangamiza vijidudu zinaweza kutibu tu ugonjwa wa kuhara uliosababishwa na vijidudu, kwa hiyo wagonjwa wengi wa kuhara hawana haja ya kutumia dawa hizo. Profesa Qian alisema:
"si magonjwa yote ya kuhara yanatokana na kuambukizwa vijidudu, kama vile mwalimu Li, ugonjwa wake huenda unatokana na tatizo la usagaji wa chakula, dawa za kuangamiza vijidudu si kama tu hazisaidii ugonjwa wake, huenda zitaleta matatizo mapya au kutatanisha zaidi."
Profesa Qian alisema, kuna wadudu wenye manufaa kwa binadamu wanaoishi tumboni, ambao wanaweza kuzuia ukuaji wa wadudu wengine wanaosababisha magonjwa. Mwalimu Li alipotumia ovyo dawa za kuangamiza vijidudu, dawa hizo pia ziliwaua wadudu wenye manufaa na kuharibu mazingira ya ndani ya mwili, kwa hivyo ugonjwa wake ulirudia mara kwa mara.
Kwa hiyo ni ngumu kwa wagonjwa kujitafutia wenyewe sababu za kuhara bila kufanyiwa upimaji na madaktari, kutumia dawa ovyo ni hatari sana, baadhi ya magonjwa ya kuhara hata yanaweza kuambukiza. Mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya matumbo katika hospitali ya No. 305 ya Beijing Profesa Huang Ping alisema:
"kama tatizo la kuhara likiendelea kwa zaidi ya siku 3 bila kupona hata kidogo, lazima mgonjwa aende hospitali, kwanza kuthibitisha kama ulipatwa na ugonjwa wa kuhara au la, unapaswa kufanyiwa upimaji wa kinyesi ili kutafuta vyanzo vya ugonjwa wako, halafu utaweza kupewa matibabu kutokana na chanzo cha ugonjwa wako."
Kama wagonjwa ambao hali yao si mbaya hawataki kwenda hospitali watafanyaje? Wataalamu walieleza kuwa wagonjwa kama hao wanaweza kunywa maji gram 500 yaliyochanganywa na gramu 10 za sukari na gramu 1.75 za chumvi. Kama tatizo lao likiondoka basi mgonjwa aache mara moja kunywa maji hayo. Wataalamu pia wanasema, tatizo dogo la kuhara linaweza kupona wenyewe baada ya siku 1 hadi 2, kama njia hii haisaidii basi wagonjwa lazima waende hospitali kupewa matibabu.
Aidha, sasa kumeingia majira ya Autumn, wakati huu ni rahisi sana kwa watoto kupatwa ugonjwa wa kuhara uliosababshwa na virusi vya aina ya rotavirus. Wataalamu walisema, virusi vya aina hiyo wanaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu, kuanzia mwezi Oktoba hadi mwezi Januari ni kipindi ambacho watu wengi hupatwa na ugonjwa wa kuhara uliosababishwa na virusi hivyo.
Hivi sasa mbali na chanjo bado hakuna dawa zinazoweza kuangamiza kwa ufanisi virusi vya aina hiyo, kwa hiyo kama watoto wakiambukizwa na virusi hivyo lazima kuwapeleka hospitali kwa wakati ili kuepusha hali yao kubadilika na kuwa mbaya.
Kutokana na kuwa hakuna dawa zenye ufanisi za kuangamiza virusi hivyo, kwa hiyo kujikinga dhidi ya virusi hivyo ni muhimu sana. Mtaalamu wa kituo cha udhibiti wa magonjwa cha China Bi. Zhang Jing alisema, virusi hivyo vinaambukiza kwa njia ya kugusana, kwa hiyo hatua muhimu za kujikinga na ugonjwa huo ni kufanya vizuri kazi za usafi.
February 14, 2018

HALF TIME: Mapishi ya slesi ya nyama ya ng’ombe na Viazi

Nyama ya ng’ombe gramu 200, kiazi kimoja?pilipili boga moja na pilipili hoho kimoja, sukari kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, mchuzi wa sosi vijiko viwili, wanga kijiko kimoja
Njia:
1. osha nyama ya ng’ombe, kata iwe slesi, changanya pamoja na chumvi, mafuta, mchuzi wa sosi, sukari, wanga.
2. kata kiazi kiwe slesi halafu weka kwenye maji, ipakue.
3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia slesi za nyama ya ng’ombe, korogakoroga, ipakue. Tia vipande vya pilipili boga na pilipili hoho korogakoroga, tia slesi za kiazi korogakoroga, tia chumvi, nyama ya ng’ombe korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
February 14, 2018

Mwanasheria mkuu wa Kenya ajiuzulu

Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai ametangaza kujiuzulu hii leo baada ya kuhudumia  kwa kipindi cha miaka 6. Kupitia mtandao wa Twitter Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Muigai ambapo amesema amepokea barua hiyo kwa masikitiko na amemshukuru kwa uongozi wake uliotukuka katika kipindi hicho cha miaka 6.
Kufuatia kujiuzulu kwa muigai Rais Kenyatta ametangaza kumteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa Paul Kihara Kariuki kuwa mwanasheria mkuu wa Taifa hilo.
Pamoja na uteuzi huo Rais Kenyatta amefanya uteuzi mwingine ambapo amemteua Kennedy Ogeto kuwa solisita mkuu katika ofisi ya mwanasheria mkuu, Abdikadir Mohammed kuwa balozi wa Kenya nchini Korea Kusini na Njee Muturi ameteuliwa kuwa Naibu Afisa anaeshughulikia ofisi ya Rais.

12 February 2018

February 12, 2018

AJALI YAUA WATANO NA WENGINE KUJERUHIWA ENEO LA KABUKU WILAYANI HANDENI

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya, baada ya basi kubwa kugongana na hiace katika eneo la Kabuku wilayani Handeni.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)  Leonce Rwegasira alisema ajali hiyo imetoke saa 5:30 asubuhi katika eneo hilo la Kabuku.
Alitaja mabasi hayo kuwa ni basi la kampuni ya AK Safari lililokuwa likitoka Lushoto kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Khalifa Mussa Omary mkazi wa Chamanzi Dar lenye namba za usajili T 497 BJB mbalo limegongana na Hiace iliyokuwa ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba T591 AKE.
Alisema waliofariki ambao ni pamoja na Dereva wa hiace aliyefahamika kwa jina moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao zimehifadhiwa Kwenye hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.
ACP Rwegasira alisema majeruhi ambao hawakuchukua majina yao kutokana na kuwasaidia kuwafikisha katika kituo cha afya Kabuku kwa ajili ya kuendelea na matibabu.
Kaimu Kamanda huyo wa Polisi alisema kuwa chanzo cha Uzembe barabarani
February 12, 2018

Mahakama kutoa uamuzi maelezo ya onyo ya Halima MdeeMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi Mosi,2018 itatoa uamuzi iwapo maelezo ya onyo yaliyotolewa polisi na mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee yapokewe kama kielelezo au la. Mdee anashtakiwa kwa kutumia lugha ya fedheha kwa Rais John Magufuli.

Awali, shahidi wa upande wa mashtaka D/SSGT Arbogast aliomba kuyatoa maelezo hayo ya onyo mahakamani kama kielelezo lakini wakili wa utetezi, Peter Kibatala alipinga akidai yalichukuliwa nje ya muda.

Hakimu mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya kusikiliza pande hizo mbili amesema Machi Mosi,2018 atatoa uamuzi iwapo maelezo hayo ya onyo yapokewe kama kielelezo au la. Mdee anadaiwa Julai 3,2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema iliyopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, alitumia lugha fedheha dhidi ya Rais.