Header Ads

Maelezo ya rais Erdoğan kuhusu Aleppo
Rais Recep Tayyıp Erdoğan afahamisha kuwa amefanya mazungumzo na rais Barack Obama wa Marekani ,rais wa Urusi Vladimir Putin na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel .
Erdoğan alizungumzia kuhusu shughui y uokoaji raia kutoka Aleppo.
Aidha pia katika ikulu ya rais rais Erdoğan alifanya mkutano na rais wa Slovenia  Borut Pahor na kujibu maswali kutoka waandishi wa habari.
Erdogan alipoulizwa kuhusu hali ya Syria alisema kuwa hali itaweza kupata suluhisho ikiwa kwanza Aleppo itaweza kuwa sawa .
Rais Erdoğan alifahamisha kuwa Uturuki na Urusi zimekuwa zikiwasliana kufanikisha shughuli ya uokoaji na kusitisha mapigano Aleppo.
Aliendelea kusema kuwa pia Uturuki imetuma mabasi amabyo yaliweza kuwaokoa raia wa Aleppo na kuwasafirisha Idlib.
Aidha wakati huo huo Erdoğan alitoa wito kwa viongozi hao kuzingatia hasa masuala ya haki za binadamu .
Kuhusu mazungumzo yake na Angela Merkel alisema kuwa walijadiliana kuhusu mambo ambayo wanaweza kushirikiana kuboresha hali ya Syria.
Obama kwa upande wake alishukuru Uturuki kwa kuonyesha ubinadamu na jambo hilo linashinikiza zaidi kwa Marekani na Uturuki kushirikiana .

Weka E-mail yako hapa upate Story

 
M-MEDIA Tz © 2016. All Rights Reserved. Powered by Massacky Media Tanzania
Top