Header Ads

Mchezaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa ni mchezaji aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani na jarida la France Football, huku Messi akiwa katika nafasi ya pili kwa msimu wa 2016-17.
Ronaldo tayari ameingiza kitita cha pauni milioni 75.62 na amempiga bao mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona ambaye amepata pauni milioni 66.12.
Fedha hizo zinatokana na mshahara, posho, malipo ya motisha na mikataba ya matangazo na Ronaldo anaonekana amepanda haraka baada ya kushinda Ballond’Or.
Mchezaji mwingine wa Barcelona, Neymar, yeye anaonekana kumpiga bao Gareth Bale wa Madrid.
Hii ndio list ya wachezaji watano wanao ingiza pesa nyingi zaidi
Cristiano Ronaldo, Real Madrid, Pauni 75.62m
Lionel Messi, Barcelona, Pauni 66.12m
Neymar, Barcelona, Pauni 47.97m
Gareth Bale, Real Madrid, Pauni 35.4m
Ezequiel Lavezzi, Hebei China, Pauni 24.63m

Weka E-mail yako hapa upate Story

 
M-MEDIA Tz © 2016. All Rights Reserved. Powered by Massacky Media Tanzania
Top