Header AdsRais John  Magufuli
Rais John Magufuli amethibitisha kuwa atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambazo kitaifa zitafanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Akizungumza kwa niaba yake, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki amesema kuwa Rais atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo,hivyo wananchi na wafanyakazi wajitokeze kushiriki na kusikiliza hotuba yake. Sadiki amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na huduma za upimaji wa afya zilizoandaliwa na taasisi za afya hivyo aliwataka wakazi wa mkoa huu na watakaofika kutumia fursa hiyo kupima afya zao.

Weka E-mail yako hapa upate Story

 
M-MEDIA Tz © 2016. All Rights Reserved. Powered by Massacky Media Tanzania
Top