Header Ads


Bao 2 ndani ya dakika 3 zimewapa Tottenham Hotspurs ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Arsenal. Hadi mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake, kipindi cha pili Spurs walikuja kwa kasi dakina ya 55 Dele Alli alifunga bao la kwanza, chini ya dakika 3 baadaye, Gabriel alimuangusha Harry Kane ndani ya boksi na refa kutoa penalti iliyofungwa na Harry Kane.
Chelsea imezidi kupaa kuelekea ubingwa baada ya kuifunga Everton goli 3-0, huku Manchester United ikitoka sare ya bao 1-1 na Swansea City. Nayo Manchester City imetoshana nguvu na Middlesbrough ya goli 2-2.

Weka E-mail yako hapa upate Story

 
M-MEDIA Tz © 2016. All Rights Reserved. Powered by Massacky Media Tanzania
Top