Header Ads

AFARIKI KWA KULA MIOGO YENYE SUMU

Mtoto wa miaka mitatu amefariki dunia, huku wanafamilia wengine 10 wakinusurika baada ya kula mihogo ya kuchemsha inayosadikiwa kuwa na sumu.

Tukio hilo lilitokea Mei 19 eneo la Mbondole Manispaa ya Ilala. Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbondole, Thomas Nyanduli alisema alipewa taarifa kuwa familia ya Chacha Fyefye yenye watu 11 ilipatiwa matibabu katika zahanati ya Kivule baada ya kula mihogo hiyo.

Nyanduli alisema wengine walihamishiwa Hospitali ya Rufaa Amana ambako baada ya matibabu waliruhusiwa kutokana na afya zao kuimarika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alithibitisha kutokea tukio hilo akisema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo.
AFARIKI KWA KULA MIOGO YENYE SUMU AFARIKI KWA KULA MIOGO YENYE SUMU Reviewed by M- MEDIA TV on May 22, 2017 Rating: 5

Recent Posts

Feat