Header Ads

Kijiji kimoja cha starehe kilicho kusini mwa Ufaransa kimekumbwa na wasi wasi baada ya zaidi ya paka 200 wa kurandaranda na wa kufugwa kufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kula sumu.

Kisa hicho kimetokea eneo la Saint Pierre la Mer kilomita 90 kutoka Kusini magharibi mwa Montpellier.

Chama cha kuwalinda wanyama kimepokea simu nyingi kufuatia kisa hicho.

Wanyama wengine na hata ndege nao walikufa baada ya kula sumu, huku kukiwa na hofu kuwa watoto huenda nao wakaila.

Chama cha paka wa kurandaranda kimeripoti matukio hayo kwa polisi kwa matumaini kuwa uchunguzi utafanywa.

"Tuna hofu kuwa mtota anawewa kuila sumu hii," mwanakijiji mmoja mwenye hofu alisema.

Weka E-mail yako hapa upate Story

 
M-MEDIA Tz © 2016. All Rights Reserved. Powered by Massacky Media Tanzania
Top