Header AdsKocha Mkuu wa timu ya soka Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amewataka wadau wa soka kuwa wavumilivu baada ya timu yake kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Rwanda katika mechi ya kufuzu mashindano ya CHAN uwanja wa CCM Kirumba mwishoni mwa wiki.

Mayanga alitoa hakikisho kuwa Taifa Stars itafuzu kwa mashindano hayo licha ya sare hiyo. Mayanga aliwapongeza wachezaji kwa bidii walioweka hata ingawa walishindwa kupata ushindi katika mechi hiyo. Hata hivyo alifichua kuwa ilikuwa tukio la kuvunja moyo kuona kikosi chake kikiruhusu wapinzani wao Rwanda kufunga bao la ugenini.

Alisema Taifa stars itarekebisha makosa waliofanya katika mechi za awali na kuhakikisha wametwaa ushindi dhidi ya Amavubi Stars ya Rwanda wakati wa marudiano

Weka E-mail yako hapa upate Story

 
M-MEDIA Tz © 2016. All Rights Reserved. Powered by Massacky Media Tanzania
Top